April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwenyekiti halmshauri; Biashara ya ngono ihalalishwe tuongeze mapato

Spread the love

UKATA wa fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida umechochea fikra mpya kwamba, biashara ya ngono inaweza kusaidia kufukia pengo hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kwenye kikao maalum cha kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichokutana kujadili na kupitisha Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2019/2020, Simon Tyosela, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iramba ameshauri kuwa, biashara ya ngono iruhusiwe ili kutanua wigo wa ukusanyaji mapato kwa halmashauri hiyo.

Tysole amewaeleza wajumbe wa kikao hicho kwamba, biashara hiyo ikihalalishwa itazisaidia halmashauri nchini kukusanya mapato kutoka kwa wanaojihusisha na biashara hiyo ‘madada poa’ jambo litalowezesha halamshauri nyingi kupumua kutokana na kunufaika na kipato.

Hoja nyingine ya Tysole kwenye kikao hicho ni kwamba, iwapo biashara hiyo itawekewa mfumo mzuri wa kulipa kodi, itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza biashara hiyo kwa kuwa, wataoshindwa kulipa kodi watalazimika kuacha kwa hiari yao.

Kauli ya Tyosela imekuja ikiwa ni baada ya ile lililotolewa na Dk. Rehema Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa Jeshi la Polisi kuwakamata madada poa wote katika mkoa wake.

Aidha, ushauri huo wa Tyosela ulipingwa vikali na wajumbe wa kikao hicho, ikiwemo Dk. Nchimbi alieleza kuwa, taifa haliwezi kuendelea kwa kukumbatia biashara hiyo, na kwamba atahakikisha anawaondoa madada poa wote katika mkoa wake.

error: Content is protected !!