Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwenyekiti bodi ya maziwa ageuka ‘bubu’
Habari Mchanganyiko

Mwenyekiti bodi ya maziwa ageuka ‘bubu’

William Ole Nasha, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Spread the love

WAJUMBE wa Baraza la Wadau wa Maziwa Tanzania wamelalamikia bodi ya maziwa kuendeshwa bila wajumbe wake kwa miaka miaka mitatu sasa, anaandika Dany Tibason.

Wametoa malalamiko hayo leo muda mfupi baada ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha, kufungua mkutano wa 13 wa baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Veta mjini Dodoma.

Dk. Aichi Kitilyi ambaye ni mwenyekiti wa bodi ameuambia mkutano huo kuwa hawezi kujibu baadhi ya hoja kwa kuwa hakuna viongozi wa bodi.

Amesema bodi yake haina viongozi na kwamba hataweza kujibu jambo lolote katika mkutano huo.
Dk. Kitilyi amesema muda mrefu bodi hiyo haina viongozi na kwamba na kwamba wameishatuma maombi kwa waziri husika.

“Kutokana na kuwa mpaka sasa bodi ya maziwa haina viongozi mimi hapa siwezi kujibu jambo lolote ambalo lilitokana na mkutano wa baraza la wadau wa maziwa ila ninaweza kutoa ushauri kama mdau wa kawaida na hii ni kwa mujibu wa sheria inayounda bodi ya maziwa” amesema Dk. Aichi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza Nathwani alivyomshambulia jirani yake

Spread the loveSHAHIDI ambaye ni fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) ameileza mahakama...

Habari Mchanganyiko

DCEA, TAKUKURU waunganisha nguvu kupamba na dawa za kulevya, rushwa

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!