September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwendokasi kubadili maisha Mbagala

Spread the love

ENEO la Mbagala na viunga vyake linatarajiwa kunufaika na mradi wa mabasi yaendayo haraka (mwendokasi) unaotarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Matumaini ya kuanza kwa ujenzi huo yametolewa na Ronald Lwakatare, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) kwamba, baadhi ya taratibu tayari zimekamilika.

Ikiwa ni hatua ya pili ya mradi wa mabasi hayo, barabara inayotarajiwa kutengenezwa ni ile itokayo Gerezani kwenda Mbagala Kuu.

Pia awamu hiyo itajenga barabara Barabara ya Chang’ombe kuanzia Mgulani kwenda kwenye makutano ya Barabara ya Kilwa na Mgulani JKT pia Barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni.

Lwakatare ameeleza kuwa, mradi wa kwanza utakuwa ni wa kilomita 20.3 katika barabara zitakazojengwa kwa Sh. 189.43 Bil na kwamba, tayari makandarasi wametia saini mkataba na Wakala wa Barabara (Tanroads).

Miongoni mwa vitu vitakavyokwenda sambamba na ujenzi huo ni pamoja na vituo vikuu vya kusimamia mabasi, karakana moja na vituo vya barabara za kupishania magari kwa gharama ya utakaogharimu Sh. 48.82 Bil.

Lwakatare amesema, ujenzi huo utaendana na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na wamiliki wa daladala kuondoa magari hayo Kituo cha Gerezani kabla ya kesho ili kupisha mradi huo.

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imeeleza kwamba, utaratibu utakaotumika kwa daladala zilizokuwa zikitumia kituo hicho ni kuwa, zile zinazopita Barabara ya Kilwa sasa zitakwenda kushusha Machinga Complex.

Daladara zinazopita Chang’ombe kuelekea Gerezani zitakwenda Mtaa wa Lindi kupitia Barabara ya Shaurimoyo na Lindi na kurudi yalikotoka kupitia barabara ya Lindi na Shaurimoyo.

Na magari yanayotumia Barabara ya Nyerere na Uhuru kuelekea Gerezani, yatakwenda kususha Mnazi Mmoja.

error: Content is protected !!