May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwendesha mashtaka akamatwa tuhuma za rushwa milioni 5

Spread the love

 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Manyara, inamshikilia Mwendesha Mashtaka wa mkoa huo, Wakili Mtalemwa Kishenyi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh.5 milioni kutokwa kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Wakili Kishenyi, alikamatwa na maofisa wa Takukuru usiku wa juzi Jumamosi, tarehe 23 Aprili 2021, akiwa amepokea kiasi hicho cha fedha.

Taarifa ya kukamatwa kwake, imetolewa leo Jumapili tarehe 25 Aprili 2021 na Holle Makungu, Mkuu wa Takukuru, Mkoa wa Manyara.

Pia, Takukuru imemtaka Mkurugenzi wa Mati Super Brands, David Mulokozi, kufika mara moja leo Jumapili Takukuru kwa mahojiano.

error: Content is protected !!