August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwanjali anyakuwa Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi

Method Mwanjali, Beki raia wa Zimbabwe anayekipiga ndani ya klabu ya Simba

Spread the love

BEKI raia wa Zimbabwe anayekipiga ndani ya klabu ya Simba, Method Mwanjali amechaguliwa kuwa mchezaji bora ndani ya klabu hiyo katika mwezi Disemba, 2016 kutokana msaada mkubwa alioutoa ndani ya kikosi hicho katika michezo iliyopita, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Mwanjali ambaye ndio msimu wake wa kwanza kuitumikia klabu ya Simba , amekuwa na msaada mkubwa katika idara ya ulinzi, na kusababisha timu hiyo kuruhusu mabao 6 katika michezo 18 ya ligi waliocheza na kufanya timu iliyoruhusu mabao machache katika ligi kuu.

Utaratibu wa kutoa zawadi ya mchezaji bora ndani ya klabu hiyo ulianza mwaka 2015 mwezi Septemba, kwa lengo la kuwapa motisha wachezaji ili waweze kujituma zaidi na kuwapa zawadi ya shilingi laki tano.

Klabu hiyo ambayo inaongoza ligi kwa sasa, muda mchache ujao watashuka dimbani katikia mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa katika uwanja wa Jamhuri uliopo Morogoro.

error: Content is protected !!