August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwandishi wa ITV aachiwa huru

Khalfan Lihundi, Mwandishi wa Habari wa ITV mkoani Arusha (katikati) muda mfupi baada ya kuachiwa huru

Spread the love

HATIMAYE Mwandishi wa Habari wa ITV, Khalfan Lihundi aliyekuwa anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Polisi cha Usa River wilayani Arumeru kwa amri ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Alexander Mnyeti kwa madai ya kuandika habari za uchochezi aachiwa huru, anaandika Mwandishi Wetu.

Kuachiwa kwake huru kumekuja baada ya jitihada kubwa za Jumuiya ya Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha (APC) chini ya Mwenyekiti wao, Claud Gwandu, ambao leo hii waliamkia kwenye kituo hicho cha polisi kufuatilia kadhia iliyomkuta Lihundi. 

Lihundi alikamatwa jana mchana kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya, awali ilikuwa afikishwe leo mahakamani lakini ukatokea utata kati ya mawakili na polisi, lakini mwisho ameachiwa kwa dhamana bila ya kufikishwa mahakamani.

 

error: Content is protected !!