Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwandishi wa habari mwingine wa uchunguzi mbaroni
Habari Mchanganyiko

Mwandishi wa habari mwingine wa uchunguzi mbaroni

Spread the love

MWANDISHI wa Habari za Uchunguzi  wa mtandao wa Watetezi TV, Jeseph Gadye anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kudaiwa kufanya uchochezi na kuchapoisha habari za uongo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa wa Watetezi wa Haki za binaadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa amesema kuwa mwandishi huyo ameitwa kuhojiwa kwenye kituo cha Polisi cha Urafiki  jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Polisi walimpigia simu Gadye ambaye ni Mhariri wa Uzalishaji Maudhui msimamizi msaidizi wa  Watetezi TV, alifikia kituoni hapo ndipo aliposhikiliwa hapo  hadi muda huu bila ya kupewa dhamana baada ya kupigiwa sdimu na askari aliyejitambulisha kuwa ni Godfrey Mkude.

Olengurumwa amesema mtandao huo unalaani vitendo vya kuwakamata waandishi wa habari kwa kuwa  vinawanyima haki ya kikatiba wanachi na wanahabari ya kupata habari na wanahabari.

“Baada ya kuchukuliwa maelezo chini ya wakili Jones Sendodo, dhamana yake ilikataliwa kwa maelezo kwamba amri ya kumkamata imetoka Iringa hivyo kituo cha polisi Urafiki wao wanamuhifadhi na baadae atapelekwa Iringa kwa ajili ya taratibu zingine”, amesema.

Amesema kuwa Mwandishi huyo amekwenda kufanya uchunguzi juu udharirishaji wa jeshi la Polisi kwa vijana sita ambao anadai kuwa wapo na wao wenyewe walilalamika pia Mkuu wa Polisi Mkoa wa Iringa alihojiwa na mwandishi huyo juu ya tukio hilo.

Taarifa ya Kituo cha Watetezi wa Haki za Binaadamu

Tarehe 17, Juni 2019, Waandishi wa habari wa Kituo cha Luninga cha mtandaoni (Online TV) cha Watetezi TV walipokea taarifa ya kuwepo kwa vitendo vya udhalilishwaji wa watuhumiwa katika Kituo cha Polisi Mafinga mkoani Iringa.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Mwandishi Joseph Gadye alifunga safari hadi mkoani Iringa kwa ajili ya kufuatilia habari hiyo kwa kufanya uchunguzi wa kutosha na mnamo Agosti 09, 2019 Watetezi TV iliripoti tukio la ukatili wa  Askari wa jeshi la polisi  katika Kituo cha Polisi Mafinga mkoani Iringa katika mitandao yake (Facebook, Twitter na You tube channel).

Katika tukio hilo inadaiwa kuwa vijana sita (Majina yao yanahifadhiwa) wakazi wa Mafinga walikamatwa na kuteswa na maofisa kwa jeshi la polisi na inadaiwa kuwa walipigwa na  kulazimishwa kulawitiana wao kwao wakiwa kituoni.

Watuhumiwa hao sita walikamatwa na jeshi la polisi mnamo mwezi Mei 19, 2019 na kushikiliwa kwa takribani siku 10 katika Kituo cha Polisi Mafinga, ambapo inadaiwa kuwa walipigwa na kulazimishwa kulawitiana wao kwa wao mbele ya maofisa wa jeshi la polisi kituo cha Mafinga wakati wakifanyiwa mahojiano.

Baada ya Watetezi TV kutoa ripoti yake sehemu ya kwanza Agosti 09, 2019 kuhusu ukatili huo, jeshi la polisi mkoani Iringa kupitia kwa Kamanda wa Polisi mkoa (RPC), ACP Juma Bwire ilikanusha taarifa hiyo na kudai kuwa ni uongo unaosambazwa mitandaoni kwa lengo la kulidhalilisha jeshi la polisi na kuichafua serikali kwa ujumla.

“Jeshi la polisi mkoa wa Iringa linaonya hao watu wanaotoa taarifa za uongo na upotoshaji zenye lengo la kudhalilisha jeshi la polisi Tanzania na serikali kwa ujumla.  Hivyo, tunatoa onyo watu wenye tabia hizo kuacha mara moja.  Aidha, nimemuagiza mkuu wa upelelezi afuatilie kwa watu wanaopotosha na kutoa taarifa za uongo. 

Pindi watakapopatikana basi hatua za kisheria zichukuliwe.  Na sasa hivi tunaendelea kufuatilia kwenye mitandao taarifa mbalimbali zikirushwa.  Kwahiyo, atakayebainika tutachukua hatua kali za kisheria,” alisema RPC Bwire katika taarifa yake na wanahabari mnamo Agosti 14, 2019.

Leo Agosti 22, 2019 Mwandishi wa habari Watetezi TV, Joseph Gandye aliyechapisha habari hiyo ametakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Urafiki, Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.

Gandye  ambaye alipigiwa simu leo majira ya saa 05.20  alifika kituoni hapo na kusubiri zaidi ya masaa 2. 

Hatimaye Mwandishi huyo alihojiwa mbele ya Wakili Jones Sendodo kwa tuhuma za kuchapisha habari za uongo mtandaoni kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Mwandishi Joseph Gandye amekamatwa rasmi katika kituo cha polisi Urafiki jijini Dar es Salaam . Mkuu wa kituo hicho amesema hawezi kumpa dhamana kwa kua hana mamlaka yoyote kwa kua aliemkamata ni polisi kutoka Iringa .

Polisi kutoka Iringa wanafanya mipango ya kumsafirisha Joseph Gandye kwenda mkoani Iringa .

Itakumbukwa mwandishi huyu ndie alietoa habari ya mwanafunzi Hosea Manga, aliechapwa na mwalimu mpaka kuvunjika uti wa mgongo mkoani Njombe.

Vilevile aliripoti kuhusu uonevu uliokua unafanywa na polisi Loliondo na kwa taarifa hiyo kupitia Watetezi TV Waziri wa mambo ya ndani Mh.  Kangi Lugola aliweza kufatilia suala hilo na kulifanyia kazi.

Mwandishi Joseph Gandye si tu miongoni mwa mwandishi mahiri bali mtayarishaji mzuri wa kipindi cha vya vipindi Haki  za Binadamu kinachorushwa live kila siku ya ijumaa saa 10 kamili jioni ndani ya studio za Watetezi TV.
5.0 WITO KWA JESHI LA POLISI MAFINGA

1. Kuzingatia haki zote za mtuhumiwa , kuto kuteswa wala kutwezwa utu wake

2. Haki ya dhamana itolewe kwa kua kosa analotuhumiwa linadhaminika.

3. Uchunguzi ufanyike kuhusu tuhuma za udhalilishwaji na uvunjwaji wa haki za binadamu unaofanywa dhidi ya watuhumiwa katika kituo hicho cha polisi.

4. Kuwaacha Waandishi wa Habari wafanye kazi zao bila kuwakamata mara kwa mara .

Imetolewa na  
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.
Onesmo Olengurumwa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!