SHAAME Simai Mcha ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, amejitosa katika kinyang’anyiro cha Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea)
Mcha amechukua fomu leo Alhamisi tarehe 25 Juni 2020, katika Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar na kuahidi endapo atapewa ridhaa ya kuwaongoza Wazanzibar, atahakikisha anaendeleza mazuri yaliyoanzishwa na Rais Ali Momahed Shein.
Amesema, ataimarisha uchumi kwa kuwekeza kwenye uvuvi ambao utatochea ajira kwa vijana.
“Nitaimarisha mapinduzi matukufu ya Zanzibar na Muungano wetu wa Tanzania,” amesema Mcha ambaye amekuwa mgombea wa 29 kuchukua fomu.

Mgombea huyo amesema, amefanya kazi maeneo mbalimbali na kwa sasa ni ofisa uhusiano wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kabla ya Mcha kuchukua fomu, ametanguliwa na Pereira Ame Silima aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuchukua fomu za kuwania Urais.
Mara baada ya kuchukua fomu, Silima amesema, Zanizbar kuna “tatizo kubwa sana na unyanyasaji la watoto na wananwake.”
“Hili limefanuyia kazi na kila aliyepita lakini matokeo hayajawa mazuri na mimi nikipita ridhaa nataka niweke mguu chini kuhakikisha tunapata ufumbuzi,” amesema.

Kwa upande wake, Iddi Hamadi Iddi amesema amejitosa kwenye mbio hizo ili kuwatumikia Wazanzibar kwani, “Urais ni dhamana, Urais siyo mapato, Urais siyo ukubwa mtu ni kushirikiana na wenzako kufuata Ilani, Katiba na miongozo ya Chama Cha Mapinduzi.”
Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji fomu hizo ni kati ya tarehe 15 hadi 30 Juni 2020. Kati ya wagombea wote 29, wanawake ni watatu.
Wagombea wote 29 waliojitokeza ni;
- Mbwana Bakari Juma
- Balozi Ali Abeid Karume
- Mbwana Yahya Mwinyi :
- Omar Sheha Mussa
- Dk. Hussein Ali Mwinyi
- Shamsi Vuai Nahodha
- Mohammed Jaffar Jumanne
- Mohammed Hijja Mohammed
- Issa Suleiman Nassor
- Profesa Makame Mnyaa Mabarawa
- Mwatum Mussa Sultan
- Haji Rashid Pandu
- Abdulhalim Mohammed Ali
- Jecha Salum Jecha
- Dk. Khalid Salum Mohammed
- Rashid Ali Juma
- Khamis Mussa Omar
- Mmanga Mjengo Mjawiri
- Hamad Yussuf Masauni
- Mohammed Aboud Mohammed
- Bakari Rashid Bakari
- Hussein Ibrahim Makungu
- Ayoub Mohammed Mahmoud
- Hashim Salum Hashim
- Hasna Atai Masound
- Fatma Kombo Masound
- Iddi Hamadi Iddi
- Pereira Ame Silima
- Shaame Simai Mcha
Leave a comment