May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwandishi TBC afariki dunia

Spread the love

MWANDISHI wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Elisha Elia amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba amesema, Elia amefikwa na mauti leo Jumamosi tarehe 24 Oktoba 2020 alipokuwa amelazwa hospitalini hapo kwa matobabu.

Dk. Rioba amesema,taarifa zaidi zitatolewa.

 

Kwa upande wake, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dk. Hassan Abbas, ametumia ukurasa wa Twitter kuomboleza kifo hicho cha Elia.

“Kwa niaba ya Serikali, tumepokea kwa masikitiko kifo cha Mtangazaji mahiri wa TBC, Elisha Elia, kilichotokea leo Dar es Salaam.”

Dk. Abbas ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema,”Elisha atakumbukwa kwa kipaji chake adhimu katika uandishi wa habari za magazeti na baadaye kuwa mtangazaji galacha.”

error: Content is protected !!