April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwandishi Erick Kabendera, azingirwa nyumbani kwake

Spread the love

MWANDISHI wa habari za kiuchunguzi, Erick Kabendera, amevamiwa na “watu wasiojulikana,” nyumbani kwake Mbweni, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa Kabendera, leo jioni watu kadhaa wakiwa na magari, walivamia nyumbani kwake na kuzingira nyumba hiyo na kuzuia mtu yeyote kuingia.

Anasema, kabla ya hapo, simu zake zote zilifungwa; na alipopiga simu Vodacom aliambiwa kuwa hayo ndio maelekezo waliyopewa na Mamlaka ya Mawasiliano ya taifa (TCRA).

Naye mtoa taarifa mmoja ameliambia MwanaHALISI ONLINE, kwamba “…inawezekana wamemchukua tayari; sababu hata simu za ndani ya nyumba hazipokelewi.”

Kabendera ni mmoja wa waandishi wa habari nchini anayeandikia magazeti mbalimbali, likiwamo gazeti la Africa Confidential linalochapishwa Uingereza.

error: Content is protected !!