Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwandishi afariki dunia saa 48 baada ya kufunga ndoa
Kimataifa

Mwandishi afariki dunia saa 48 baada ya kufunga ndoa

Spread the love

 

MWANDISHI wa habari na mfanyabiashara maarufu nchini Malawi, Russell Chimbayo amefariki dunia siku mbili baada ya kufunga ndao na mchumba wake, Jacqueline Joanna. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea).

Wawili hao, walifungwa ndao hiyo tarehe 2 Oktoba 2021, katika Kanisa la Mtakatifu James, Zingangwa nchini humo na baadaye jioni, hafla ikafanyika mjini Blantaya, Mtendere Garden.

Taarifa kutoka Malawi zinaeleza, Chimbayo alifikwa n amauti jioni ya Jumatatu lakini taarifa za kifo chake zilianza kusambaa juzi Jumanne. Inaelezwa alifikwa n amauti baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Enzi za uhai wake, mwandishi huyo alifahamika kwa ubunifu wa kuandaa vipindi mbalimbali.

Kingsley Mtila ambaye ndiye aliyeongoza sherehe hiyo alisema “ni Jumamosi iliyopita tu nilikuwa mshereheshaji wa harusi yako, lakini Jumatatu jioni dada yako alinipigia simu akisema haupo tena, pumzika kwa amani Russell.”

Kwa upande wake, Laura Munthali amesikitishwa na kifo hicho akisema “nimeamka na kukutana na taarifa mbaya ya kifo chako. Ulikuwa rafiki yangu mkubwa. Tumetoka mbali na ni miezi miwili imepita tangu usherekee shahada yako na tarehe 2 Oktoba 2021, tulisherekea ndoa yako sasa hatupo nawe.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!