Tuesday , 21 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwanaye Museveni: Nimechoka kusubiri, nitagombea urais 2026
Kimataifa

Mwanaye Museveni: Nimechoka kusubiri, nitagombea urais 2026

Spread the love

MTOTO wa kiume wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema  akiwa kama kijana amechoka kusubiri na sasa atagombea kiti cha urais wa Taifa hilo mwaka 2026. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Muhoozi ambaye pia ni Mkuu wa zamani wa Jeshi la Ardhini la Uganda ametoa tangazo hilo katika ujumbe wake wa Twitter jana Jumatano, akisema kuwa watu wamekuwa wakimtaka atoe tangazo hilo.

Muhoozi mwenye utata ambaye mara kwa mara amekuwa akiibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kauli zake, ameandika hivi; “Mmenitaka mimi kulisema! Sawa, kwa jina la Yesu Mungu wangu, kwa jina la vijana wote wa Uganda na dunia na kwa jina la mageuzi bora, nitagombea Urais katika mwaka 2026!” alituma ujumbe wa Twitter na kuongeza;

“Fidel Castro shujaa wangu alikuwa Rais akiwa na umri wa miaka 32, ninakaribia kufikia miaka 49, sio sawa kabisa kutokuwa rais, vijana wanapaswa kuwa marais wa mataifa yao.

“Nani anakubaliana nami kwamba muda wetu vijana umewadia? Inatosha sasa kuendelea kuongozwa na wazee na kututawala ni muda wa vijana kung’aa,” ameandika.

Ametolea mfano kuwa waziri mkuu wa Uingereza ana miaka 42, waziri mkuu Finland ana miaka 37 ilihali yeye anakaribia kufikisha miaka 50, “tumechoka kusubiri nitasimama kugombea,” amesema.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Xi Jinping awasili Urusi, kufanya mazungumzo na Putin

Spread the love  RAIS wa uchini Xi Jinping amewasili sasa nchini Urusi,...

Kimataifa

Maandamano Kenya, Afrika Kusini yashika kasi, wapinzani wakishikiliwa

Spread the love  MAANDAMANO ya kupinga serikali zilizoko madarakani nchini Kenya na...

Kimataifa

Maandamano Afrika Kusini: Tanzania yatahadharisha raia wake

Spread the love  WAKATI maandamano yaliyoitishwa na Chama cha upinzani Afrika Kusini,...

Kimataifa

ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa rais Vladmir Putin wa Urusi

Spread the love  MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita (ICC) imetoa...

error: Content is protected !!