Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwanaume mrefu zaidi Marekani afariki dunia
Kimataifa

Mwanaume mrefu zaidi Marekani afariki dunia

Spread the love

 

MWANAUME mrefu zaidi nchini Marekani aliyejulikana kwa jina la Igor Vovkovinsky, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 38 kutokana na ugonjwa wa moyo. Anaripoti, Mwanaharusi Abdallah TUDARCo …. (endelea).

Vovkovinskiy mwenye asili ya Ukraine, alizawa tarehe 8 Septemba, 1982 na mama yake Svetlana Vovkovinska na baba yake Oleksandr Ladan mjini Bar nchi humo.

Hata hivyo, mwaka 1989 familia yake ilihamia katika mji wa Rochester huko nchini Marekani wakitafuta matibabu ya uvimbe uliokuwa umeathiri tezi yake.

Vovkovinsky ambaye alikuwa na urefu wa futi 7 na inchi 8.33 (sawa mita 2 na sentimita 34.5), alifariki dunia wiki iliyopita katika kliniki ya Mayo nchini Marekani wakati akipatiwa matibabu ya moyo.

Mama yake kijana huyo ambaye pia muuguzi wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika kliniki hiyo ya Mayo, alithibitisha kifo hicho cha mwanaye kwenye mtandao wa Facebook.

Vovkovinskiy aliingia kwenye kitabu cha historia ya ‘Guinness Book of Records’ mwaka 2010 kwa kuwa mwanamume mrefu zaidi nchini Marekani kipindi hicho akiwa na umri wa miaka 27.

Nguli huyo alishinda mashindano ya Guinness baada ya kumpiku ofisa wa polisi wa Virginia, George Bell kwa urefu wa nchi tatu.

Kutokana na urefu wake, Vovkovinskiy alikuwa akipata ugumu wa kusafiri na kupata viatu vya saizi yake.

Mwaka 2012, aliwaomba wasamaria wema kumchangia dola za Marekani 16,000 kulipia viatu maalum kwa sababu vingine vilikuwa vikimuumiza na kupitia mchango huo alioupokea ulimsaidia kutengenezewa viatu maalumu na kampuni ya Reebok.

Lakini pia kijana huyo alijizolewa umaarufu mkubwa katika kampeni ya Rais Obama ambapo alivaa T-sheti iliyochapishwa “Mfuasi mkubwa wa Obama Duniani’’ tukio ambalo lilizua mjadala katika vyombo vya habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!