Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwanasiasa wa upinzani Eswatini auawa kwa kupigwa risasi
Kimataifa

Mwanasiasa wa upinzani Eswatini auawa kwa kupigwa risasi

Spread the love

 

WATU wenye silaha nchini Eswatini wamedaiwa kumuua mwanasiasa mashuhuri wa upinzani na mwanasheria wa haki za binadamu, Thulani Maseko nyumbani kwake juzi tarehe 21 Januaria, 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Tukio hilo linadaiwa kujiri saa chache baada ya mfalme wa nchi hiyo, Mswati wa tatu kuwashutumu wanaharakati wanaopinga utawala wake.

Maseko aliuawa kwa kupigwa risasi Jumamosi usiku na washambuliaji wasiojulikana huko Luhleko, umbali wa kilomita 50 na mji mkuu Mbabane.

Msemaji wa chama cha upinzani, Sikelela Dlamini amesema wauaji walimpiga risasi kupitia dirisha akiwa ndani ya nyumba na familia yake.

Serikali ilituma salamu za rambirambi kwa familia yake, ikisema kifo cha Maseko ni “hasara kwa taifa” na kwamba polisi wamekuwa wakiwasaka waliomua.

Maseko alikuwa mwanasheria kiongozi wa haki za binadamu na mwandishi wa maoni nchini Eswatini, ambaye alikuwa na kesi inayoendelea mahakamani dhidi ya uamuzi wa Mfalme Mswati wa tatu kubadili jina la nchi na kuipa jina la Eswatini kwa amri.

Jina la nchi lilibadilishwa kutoka Swaziland na kuitwa Eswatini kwa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 2018.

Msimamo wa Maseko ulikuwa kwamba Mfalme hakufuata utaratibu wa katiba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!