August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwanasheria, mhandisi wa Jiji Mwanza kizimbani

Spread the love

HALMASHAULI ya Jiji la Mwanza leo imesimamisha kazi watumishi wawili kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kusababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. 300 milioni, anaandika Moses Mseti.

Waliosimamishwa kazi ni Ezekiel Kunyaranyara, Mhandisi na Makusudi Bwabo, Mwanasheria wa Jiji.

Kunyaranyara anatuhumiwa kusimamia vibaya fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa kwa ajili ya matengenezo ya dharura.

Bwabo anatuhumiwa kutokana na kulalamikiwa na wafanyabiashara kwamba wakati wa kukusanya mapato katika biashara zao, huwatisha na hata kuwapeleka mahakamani bila sababu za msingi.

Miradi anayotuhumiwa kusimamia wakati wa ukarabati na kuwa chini ya kiwango ni jengo la machinjio liliopo Nyakato, Kata ya Mhandu, Daraja la Mwananchi lililopo Kata ya Mahina, mitaro ya barabara za Kata za Mhandu, Mkuyuni, na ukarabati wa kituo cha kulelea watoto waisho katika mazingira magumu.

Adamu Mgoyi, Mkurugenzi wa Jiji, na James Bwire, Meya wa Jiji, wamethibitisha kuwa wamesimamisha watumishi hao kwa tuhuma hizo.

Bwire amesema mhandisi huyo ameshindwa kuonesha uzalendo wa kusimamia miradi hiyo, badala yake imetekelezwa chini ya kiwango.

Ametoa mfano wakituo cha kulelea watoto wasiojiweza, kuwa kilipaswa kukarabatiwa kwa Sh. 19 milioni lakini ukarabati uliofanywa ni upakaji wa rangi pekee.

“Huyu mhandisi mwenyewe ndiye aliyependekeza na kuomba fedha hizo kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho, lakini Sh. Milioni 19 zimetumika kwa kukapaka rangi, chokaa na kutengeneza milango miwili tu, badala ya kukarabati sehemu zilizoelekezwa,” amesema Bwire.

error: Content is protected !!