MWANAMUZIKI nchini India apiga gitaa kwenye meza ya kufanyia upasuaji ili kuwasaidia madaktari kutibu mishipa (involuntary muscle spasms) katika vidole vyake, anaandika Jovina Patrick.
Abhishek Parasad aliombwa na madakdari kupiga gitaa kila wakati walipokuwa wanatibu tatizo hilo linalojulikana kama “musician’s dystonia” katika ubongo wake.
Tatizo hilo katika mishipa ya Prasad ilimzuia kutumia vidole vyake, katika mkono wake wa kushoto wakati akipiga gitaa.
Prasad mwanzo alidhani tatizo hilo linasababishwa na mazoezi ya mara kwa mara ya kupiga gitaa. Akajaribu kupumzika kwa muda lakini alipoanza kupiga gitaa hali ikawa vile vile.
Prasad anasema,“Baadhi ya madaktari waliniambia ni matatizo madogo tu katika mishipa, nikikapewa dawa za kutuliza maumivu, lakini hali haikubadilika.”
Daktari Shahara Srinivasan alimshauri kufanya upasuaji mara baada ya kugundua ana tatizo la “musician dystonia” na kumtoa hofu kuwa itakuwa sawa.”nilishauriwa kufanya upasuaji wa ubongo lakini nilikuwa mwoga sana. Daktari Shahara Srinivasan alinitia moyo” alisema Prasad.
Anasema baada ya upasuaji wiki moja baadaye vidole vyake vilifunguka na kurudi katika hali ya kawaida.
Leave a comment