September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwanamke mbaroni kwa kugoma kurejesha mamilioni ya fidia aliyolipwa kimakosa

Spread the love

MWANAMKE mmoja raia wa Kenya amegoma kurejesha kiasi cha Sh milioni 152 alichowekewa kimakosa kwenye akaunti yake ya Benki na Mfuko wa fidia kwa waathiriwa wa shambulizi la kigaidi katika Ubalozi wa Marekani mwaka 1998 jijini Nairobi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Marry Ngunyi Muiruri aliwekewa fedha hizo kimakosa katika Benki ya Nairobi nchini Kenya ilihali mtu halisi aliyetakiwa kuwekewa fedha hizo ni Marry Njoki Muiruri.

Kutokana na mkanganyiko huo, mwanamke huyo alitakiwa kurejesha fedha hizo lakini aligoma kwa madai kuwa naye pia alistahili kulipwa fidia hiyo.

Mfuko huo umeomba mahakama kuu nchini humo itoe amri ya kurejeshwa kwa fedha alizopokea Mary kiasi cha dola za Marekani 65,683.50 ( Tsh milioni 152) Novemba mwaka 2020..

Mfuko huo uliomba Benki hiyo ya Nairobi kurejesha pesa hizolakini mwanamke huyo alikataa kuridhia ombi hilo.

Aidha, imelezwa kuwa hadi Mahakama ilipotoa agizo kwa Mfuko huo kwamba Benki hiyo ya Nairobi, ifungie akaunti ya Marry Februari, 2021 tayari mwanamke huyo alikuwa ametoa kiasi kikubwa cha pesa na kubakisha Sh milioni 13 pekee.

Wakenya kadhaa waliwasilisha kesi katika Mahakama za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Sudan na Iran kati ya 2008 na 2012 wakitaka walipwe fidia kwa majeraha na kupoteza jamaa zao katika shambulio la bomu la Agosti ,1998 katika Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi.

error: Content is protected !!