July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwanamke anayetuhumiwa kumchomea ndani kwa petroli mpenzi wake akamatwa

Spread the love

 

POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Grace Janes Mushi (25), kwa tuhuma za kumchoma moto ndani ya nyumba aliyekua mpenzi wake, Khamis Abdallah (25). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana Ijumaa tarehe 16 Julai 2021, majira ya saa 8:30 usiku, maeneo ya Mbezi Makabe kwa Mzungu Wilaya ya Ubungo.

Amesema, mtuhumiwa Grace majira hayo ya saa nane usiku aliamka na kumfungia mlango kwa nje Khamis Abdallah kisha kumwagia mafuta ya petroli nyumba hiyo, kitendo kilichosababusha Khamisi kuungua na  kufariki dunia akiwa ndani.

Kamanda Muliro amesema, uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kimapenzi.

error: Content is protected !!