July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwanahabari auawa kwa risasi

Spread the love

HASSAN Hanafi, mwanahabari aliyesaidia kundi la Al-Shabaab kuua wanahabari wenzake nchini Somalia ameuawa, anaandika Happiness Lidwino.

Shirika la Habari la Uingereza (BBC) limeripoti kuwa, Hanafi ameuawa kwa kupigwa risasi mapema leo baada ya kuhukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi nchini humo.

Hanafi alipatikana na hatia ya kushiriki katika mauaji ya Sheikh Noor Mohamed Abkey (mhariri wa Shirika la Habari la SONNA), Sa’id Tahlil Warsame, (Mkurugenzi wa HornAfrik, Mukhtar Mohamed Hirabe, Mkurugenzi wa Radio Shabelle na wanahabari wengine.

Alikamatwa nchini Kenya Agosti mwaka 2014 na kupelekwa Somalia mwishoni mwa mwaka jana. Ambapo alihukumiwa kifo na Mahakama ya kijeshi ya ngazi ya chini ya nchini Somalia tarehe 3 Machi mwaka huu.

Kwa mujibu wa shirika hilo, mwanahabari huyo alikiri kuhusika na mauaji ya wanahabari watano.

Hanafi ambaye ni mwanachama wa kundi la al-Shabab alikamatwa nchini humo Agosti mwaka jana akiwa kwenye harakati za kutoroka.

Upande wa mashtaka ulimshtumu kwa kuhusika na mauaji ya waandishi wengine maarufu nchini Somalia mwaka 2007.

Hanafi alijiunga na wapiganaji wa kundi la al-Shabab miaka michache iliopita baada ya kufanya kazi na Redio Andalus ambayo ndio inayotoa taarifa za kundi hilo.

Abdinoor Aden, Mwandishi wa BBC anasema Hanifa alikuwa maarufu kwa wasikilizaji wengi wa redio nchini Somalia baada ya kujiunga na idhaa maarufu ya Quran FM. Aliondoka mwaka 2006 na kujiunga na mtandao huo.

error: Content is protected !!