January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwanafunzi UDSM afariki dunia kwa kujirusha ghorofani

Spread the love

 

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania, Manawa Horera (22) amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Jana Jumanne, tarehe 11 Januari 2022, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema tukio hilo limetokea saa 4:30 usiku juzi Jumatatu eneo la Hostel za Magufuli, Ubungo Dar es Salaam.

Alisema Manawa alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili kitivo cha shahada ya uhasibu ambapo mwanafunzi huyo aliingia kwenye chumba cha mwanafunzi mwenzake Hamza Abdulhaman kisha kuiba kompyuta mpakato ‘laptop’ aina ya HP.

Kamanda Muliro alisema, Manawa alipoonekana na wanafunzi wenzake, “aliamua kuruka kupitia dirishani kutoka ghorofa ya pili kulipo chumba hicho na kudondoka chini ikapelekea kuumia maeneo mbalimbali ya mwili wake.”

Alisema, baada ya kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili “lakini alifariki dunia.”

“Jeshi la Polisi linawataka wanafunzi kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwani maenei hayo ya Hostel yamekuwa na malalamiko ya wanafunzi laptop zao kuibiwa na watu wanaodhaniwa ni wanafunzi laptop zao kuibiwa na watu wanaodhaniwa ni wanafunzi wenzao swala ambalo linaweza kukatisha masomo yao ikibainika ni wahalifu,” alisema

error: Content is protected !!