Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwanafunzi apeleka kuku shuleni kama malipo ya karo
Kimataifa

Mwanafunzi apeleka kuku shuleni kama malipo ya karo

Spread the love

 

MWANAFUNZI Lawrence Murimi mwenye umri wa miaka 14, anayetaka kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya Upili ya Kangaru kaunti ya Embu nchini Kenya,amewasili shuleni hapo akiandamana na mamake huku akiwa amebeba kuku kwenda kulipia karo ya shule ya upili. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Akizungumza mwanafunzi huyo, siku ya jumatano tarehe 18 mei 2022 kuwa walisafiri kilomita 5 hadi kufika shuleni akiwa na mamake,Lawrence anasema alitokwa na machozi,baada ya kurudishwa nyumbani kwenda kuchukua pesa ksh 48000, zinazotakiwa kwa ajili ya kulipia karo ya shule.

‘’Nilimwambia mama kwamba huyu kuku niliyopewa ndiye ambaye tunaweza kumpeleka shuleni, kwaajili ya kulipia karo shuleni,hata hivyo baaada ya kujaribu kugonga milango yote ili kutafuta msaada bila mafanikio,’’alizungumza wakiwa nje ya lango la shule.

Aliongeza kuwa huyo kuku alikuwa na thamani ya Ksh1000, ikiwa ni fedha kidogo ikilinganishawa na karo inayofaa kulipia katika shule hiyo,ili aweze kusajiliwa.

Hata hivyo kulingana na tovuti ya the Citizen nchini Kenya ,imesema kuwa Lawrence Murimi alipata alama 313 katika mitihani yake ya KCPE, mwanafunzi huyo alipewa jogoo na mjomba wake kama zawadi.

Mamake Lawrence amesema kuwa baada ya kupokea barua ya kusajiliwa kwa mwanawe, alianza kuzunguka ofisi zote ili kutafuta msaada lakini hakufanikiwa.

Anasema kuwa mwanawe alilazimika kwenda shule ya upili na daftari alizokuwa akitumia,katika darasa la nne.

Aidha mama huyo anayetoka katika mtaa wa Majengio huko Embu,sasa anawaomba wasamaria wema kumsaidia mwanawe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!