Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Mwanafunzi amwaga machozi akizungumza na Rais Samia kwa simu ‘live’
Elimu

Mwanafunzi amwaga machozi akizungumza na Rais Samia kwa simu ‘live’

Spread the love

 

Mwanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Skondari Benjamini Mkapa iliyopo jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mzena amemwaga machozi baada ya kuzungumza na Rais Samia Suluhu Hassan mubashara kwa njia ya simu kumtakia Kheri ya kuzaliwa kwake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwanafunzi huyo ambaye ni mmoja wa wanafunzi wenye uhitaji maalum amezungumza na Rais Samia leo tarehe 27 Januari, 2022 katika hafla ya pongezi za siku ya kuzaliwa kwa Kiongozi huyo mkuu wa nchi kutoka kwa wanafunzi hao.

Katika hafla hiyo ambayo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Samia ambaye amefikisha umri wa miaka 62, imeibua furaha ya kipekee kwa wanafunzi hao waliokata keki na kuwalisha viongozi wako kama ishara ya kusherehekea siku hiyo.

Akizungumza na wanafunzi hao kwa njia ya simu ya mkononi Rais Samia alimuahidi Emmanueli kuwa ataitembelea shule hiyo katika siku za usoni na kuzungumza na wanafunzi hao.

Kauli hiyo ya Rais Samia imekuja baada ya Emmanueli kumuomba kiongozi huyo, aende Ikulu kumtembelea ili azungumze naye.

“Nikiwa Dar es Salaam nitakuja kutembelea shule ya Benjamini Mkapa,” alijibu Rais Samia na kushangiliwa na wanafunzi hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

error: Content is protected !!