February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwanafunzi aliyetumbukia chooni aokolewa, Polisi kuchunguza

Spread the love

MWANAFUNZI wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Seliani iliyoko wilayani Arusha, Emanuel Zacharia amenusurika kifo baada ya kutumbukia katika shimo la choo cha shule hiyo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Ramadhan Ng’azi amethibitisha tukio hilo akisema kuwa, lilitokea asubuhi ya leo tarehe 26 Oktoba 2018, majira ya saa tatu na nusu asubuhi.

Akizungumza na mtandao huu, Kamanda Ng’azi ameeleza kuwa, Zacharia alipatwa na mkasa huo alipokwenda chooni kujisaidia, ambapo isivyo bahati shimo la choo lilitumbukia.

Ameeleza kuwa, baada ya tukio hilo kutokea, wananchi, waalimu na polisi walifanya jitihada za kumuokoa mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa yuko katika Hospitali ya Seliani akipatiwa matibabu.

Kamanda Ng’azi amesema Jeshi la Polisi linachunguza chanzo cha tukio hilo, na kutoa saa tatu kwa uongozi wa shule hiyo kufanya marekebisho ya choo hicho.

error: Content is protected !!