March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwamuzi Simba vs Yanga huyu hapa

Mashabikiwa timu za Simba na Yanga

Spread the love

JONESIA Rukyaa kutoka Kagera ametangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kuwa mwamuzi wa kati kwenye mechi ya Simba na Yanga itakayofanyika Jumapili wiki hii. Anaandika Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mechi hiyo ya watani wa jadi itapigwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Wasaidizi wengine kwnenye mechi hiyo ni Mohammed Mkoni wa Tanga na Fednand Chacha kutoka Mwanza.

Leo tarehe 26 Septemba 2018, Clifford Ndimbo ambaye ni Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF amesema, waamuzi hao wametajwa mapema ili waweze kukuana ambapo Elly Sasii wa Dar es Salaam atakuwa mwamuzi wa akiba huku Kamishna wa mechi hiyo akitajwa John Komba kutoka Dodoma.

Amesema kwamba, mechi hiyo itachezwa saa 10:00 Alasiri.

error: Content is protected !!