August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwambe kumrithi Kairuki TIC

Spread the love

JOHN Magufuli, Rais wa Tanzania leo amefanya uteuzi mpya Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), anaandika Hamisi Mguta.

Awali nafasi hiyo ilikuwa chini ya Juliet Kairuki ambaye alitenguliwa na Rais Magufuli Aprili 24, mwaka huu baada kupatikana kwa taarifa kuwa tangu alipoajiliwa mwaka 2013 kiongozi huyo alikuwa hachukui mshahara wa serikalini.

Kabla ya uteuzi huo Mwambe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida ambapo anatakayechukua nafasi hiyo atatajwa baadaye.

Katika hatua nyingine Rais amemteua Clifford Tandari aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezazji Tanzania kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro nafasi ambayo ilikuwa chini ya John Ndunguru ambaye amestaafu.

error: Content is protected !!