Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mwalimu: Tujiandae kisaikolojia kuongozwa na Lissu
Habari za Siasa

Mwalimu: Tujiandae kisaikolojia kuongozwa na Lissu

Salum Mwalimu, Mgombea Mwenza wa Urais Tanzania kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

MGOMBEA mwenza wa urais kupitia Chadema, Salum Mwalimu amewaomba Watanzania kufanya uamuzi juu ya maisha yao katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika kesho tarehe 28 Oktoba 2020 badala ya kulalamika juu ya changamoto wanazokabiliana nazo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwalimu ametoa ombi hilo leo Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020 katika mkutano wa kufunga kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa Chadema, Tundu Lissu uliofanyika Uwanja wa Tanganyika Packres jijini Dar es Salaam.

“Muda wa kulalamika umepita, muda wa kusikitika umekwisha, muda wa kupiga kelele chini kwa chini umepita, sasa ni muda wa kufanya maamuzi. Tumeumizwa miaka mitano, tumeaminishwa demokrasia inachelewesha maendeleo kumbe uongo, sasa basi,” amesema Mwalimu.

Mwalimu amesema, wananchi wajitokeza kwa wingi kesho kupiga kuraili kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema

“Waliamini Rais John Magufuli hawezi kung’oka, wamejidanganya kwelikweli Magufuli ameshaanguka, ni kwenda kumaliza kazi kesho, wanaosema haiwezekani inawezekana. Watanzania tushikamane kwa umoja wetu tuyakatae maisha ya miaka 5 iliyopita twende tukajenge Tanzania mpya,” amesema Mwalimu.

“Inawezekana siku moja kuamka CCM haiko madarakani na Magufuli hayuko Ikulu, vyombo vya dola jiandaeni kisaikolojia kwamba rais anayekuja ni Tundu Lissu. Wote tujiandae kisaikolojia kuongozwa na Lissu,” amesema Mwalimu.

Mwalimu amesema, yeye na Lissu wamejipanga kuleta mabadiliko nchini Tanzania endapo watashinda uchaguzi huo.

“Tumejipanga mimi na Lissu, tumejipanga sawasawa, tuna dhamira njema juu ya taifa mama Tanzania,  tunataka tuwahakikishie tunairudisha  kwenye mstari, kuona Tanzania ikiishi katika utaratibu na misingi ya haki na maendeleo ya Watanzania,” amesema Mwalimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!