May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwalimu mkuu adaiwa kuchukua rushwa laki nne ili mwanafunzi asiendelee na masomo

Spread the love

 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma, leo Jumatatu, tarehe 19 Julai 2021, inamfikisha mahakama Maliselo Kapampa Saveli (29), kwa tuhuma za kupokea rushwa Sh.400,000. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Saveli ambaye ni Kaimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mafurungu na pia ni Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Ilangali kilichopo Kata ya Manda wilaya ya Chamwino, aliomba rushwa ya Sh. 600,000 na kupokea Sh.400,000.

Taarifa ya Sosthenes Kibwengo, Mkuu wa Takukuru, Mkoa wa Dodoma, aliyoitoa leo Jumatatu imesema, Saveli atafikishwa mahakamani na kumfungulia mashtaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya mwaka 2019.

Amesema, Savela anadaiwa kupokea rushwa hiyo kutoka kwa mtoa taarifa wao ili asimchukulie hatua kwa kitendo cha utoro wa mtoto wake ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mafurungu.

Kibwengo amesema, ”elimu ni ufunguo wa maisha na Serikali yetu inafanya juhudi kubwa kuimarisha mazingira ya utoaji elimu ikidhamiria kuwa huduma bora za elimu ziwafikie wananchi wote.”

”Kitendo cha Mwalimu mmoja kudiriki kuomba na kupokea rushwa ili kukwamisha malengo hayo ikiwa ni pamoja na kuenenda kinyume na taaluma yake kwa kukwamisha badala ya kuchochea elimu ni kitendo dhalili na ni kinyume na mienendo ya walimu wengi wa mkoa wetu wa Dodoma,” amesema

Mkuu huyo wa Takukuru ametoa wito akisema ”tunawataka walimu na wazazi wa wanafunzi mkoani Dodoma kuendelea kusisitiza umuhimu wa elimu na kamwe kutojiingiza kwenye vitendo vya rushwa na tabia nyingine za utovu wa maadili kwani rushwa hailipi.”

error: Content is protected !!