Saturday , 22 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwalimu, mhasibu wafikishwa mahakamani kwa rushwa
Habari Mchanganyiko

Mwalimu, mhasibu wafikishwa mahakamani kwa rushwa

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imemfikisha mahakamani mwalimu mkuu wa shule ya mingi Msisi iliyopo jijini Dodoma, David Isaac Mdek kwa kesi ya jinai namba 52/2019 na kesi hiyo imefunguliwa Januari 25 mwaka huu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akimsomea mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini Denis Mperembwe Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Clarence Kimaro aliiambia Mahakama kuwa Mshtakiwa ametenda makosa ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22, Matumizi mabaya ya madaraka kinyume na Kifungu cha 31, ubadhirifu kinyume na Kifungu cha 28 vyote chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Alisema kuwa makosa mengine ni kughushi nyaraka kinyume na Kifungu cha 333, 335(a), na 337 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu (Sura 16 Rejeo la 2002) na Udanganyifu kwa njia ya nyaraka kinyume na kifungu cha 342 Sheria ya Kanuni za Adhabu (Sura 16 Rejeo la 2002).

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Mshitakiwa ambaye ni Mwalimu Davidi Isaac Mdeka kati ya Septema 1, 2015 na Septemba 21, 2015 aliandaa Muhtasari wenye saini za wajumbe wa Kamati ya Shule ya Msingi Msisi na kuidhinisha kutolewa fedha kiasi cha Tshs 1,000,000 (Milioni moja tu) toka Benki ya NMB Tawi la Dodoma kwa ajili ya ukarabati wa choo huku akijua kuwa Muhtasari aliowasilisha benki ni wa kughushi.

Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana na kesi imehairishwa hadi tarehe 20/02/2019 ambapo kesi itakuja kwa ajili ya kutajwa.

Aidha katika hatua nyingine TAKUKURU Wilaya ya Mpwapwa Januari 24 mwaka huu iliwafikisha mahakamani na kuwafungulia kesi ya jinai namba 20/2019, Idani Tangasi Mugomela aliyekuwa mhasibu wa halmashauri ya Mpwapwa na Happyness Mkeni aliyekuwa mhasibu halmashauri ya Wilaya  ya Mpwapwa kwa sasa ni Mhasibu Halmashauri ya Morogoro Vijijini.

Akiwasomea mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Paschal Mayumba, Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU, Hilda Soko aliieleza Mahakama kwamba washitakiwa wakiwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Kitengo cha Uhasibu walitenda kosa la kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22, Ubadhirifu kinyume na Kifungu cha 28 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007 pamoja na kughushi kinyume na kifungu cha 335 cha sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16 rejeo la 2002.

Washtakiwa waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti. Kesi hii imehairishwa hadi tarehe 12 Februari, 2019 itakapotajwa tena.

Aidha TAKUKURU Mkoa wa Dodoma inawakumbusha watumishi na wananchi kufuata sheria na kujiepusha na vitendo vya rushwa na kueleza kuwa wote wanaojihusisha na rushwa mkono wa sheria hautawaacha salama. Tunawaomba wananchi wazalendo wawafichue wanaojihusisha na vitendo vya rushwa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Naye Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Musa Chaulo alisema kuwa taasisi hiyo itaendelea na mapambano juu ya vitendo vya rushwa kwa mtoaji na mpokeaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

Spread the loveBARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari Mchanganyiko

Upandaji miti uzingatie kuondoa umaskini kwa wananchi

Spread the loveKATIBU Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk. Musa Ally Musa...

error: Content is protected !!