Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mwalimu amjaza mimba ‘denti’ afungwa miaka 30
Habari Mchanganyiko

Mwalimu amjaza mimba ‘denti’ afungwa miaka 30

Spread the love

MJENGI Samson, Mwalimu wa Shule ya Msingi Isomya, Manispaa ya Singida, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kumbaka na kumjaza mimba mwanafunzi wa darasa la sita katika shule hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Hukumu hiyo imetolewa na Aristida Tarimo, Hakimu Mfawidhi wa Wilaya baada ya mwalimu huyo kutiwa hatiani pasipo na shaka.

Samson amehukumiwa kwa makosa mawili ambapo, kosa la kwanza, ni la kumbaka mtoto huyo hivyo ametupwa jela kwa miaka 30, kosa la pili ni kumjaza mimba ambapo amefungwa miaka miwili, adhabu hizo zitaenda sambamba.

Patricia Mkina ambaye ni mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo ameeleza, katika shauri hilo la jinai, tukio la kwanza lilifanyika kati ya tarehe 4 Aprili 2019 na Julai 2019.

Mkina ameleza, Samason alimfanyia unyama mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16 katika Kijiji cha Isonya, Kata ya Mwankoko.

Awali, mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo, lakini baada ya kupelekwa ushahidi ikiwa ni pamoja na mwanafunzi mwenyewe kuieleza mahakama, mtuhumiwa huyo alikuwa akimpeleka vichakani kutenda tendo hilo.

Na hata baada ya kupimwa na madaktari kama alikuwa na ujauzito, mtoto huyo alipoulizwa muhusika, alimtaja mwalimu huyo.

“Baadaya kumtaja mwalimu Samson kwamba ndiye aliyehusika, wazazi wake walikwenda kutoa taarifa kwa mtendaji kata, mkuu wa shule na kituo cha polisi,” ameeleza Mkina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!