January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwalim aonya watangaza nia Chadema

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Salum Mwalim

Spread the love

UONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ngazi ya taifa umekutana na watangaza nia katika ngazi ya ubunge Kanda ya Kati. Anaandiaka Dany Tibason … (endelea).

Hata hivyo, chama hicho kimetahadharisha kuwa, hakitasita kuwachukulia hatua kali wale wote ambao watabainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Akizungumza na watia nia katika kanda hiyo Naibu Katibu Mkuu Chadema visiwani Zanziba, Salum Mwalimu alisema, hakuna mtu yeyote ambaye atapata nafasi ya uongozi ndani ya chama kwa kutoa rushwa.

Mwalimu alisema kamwe chama hakitasita kumfukuza uanachama au kulikata jina la mgombea yeyote ambaye atabainika kuwa amepitishwa kwenye kura za maoni kwa kutumia hongo.

“Tunajua wazi kuwa wapo baadhi ya watia nia ambao wamewakamata vilivyo viongozi wa kanda au mikoa ili waweze kuwapitisha katika kura za maoni.

“Hatuwezi kuwa na wagombea ambao wanakubalika ndani ya chama kwa sababu ya kutoa rushwa kama ilivyo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na badala yake tunahitaji wagombea ambao wanakubalika nje ya chama.

Mbali na hilo amesema, kwa sasa Chadema inajiandaa kuingia Ikulu huku akisema iwapo chama hicho kitashika dola hakina mpango wa kulipiza kisasi kwa wale ambao walionekana kukitaabisha chama hicho.

“Pamoja na kuwa hatuwezi kulipiza kisasi lakini, kuna baadhi ya idara ambazo watendaji wake hawafanyi kazi kwa viwango vinavyotakiwa hivyo ni lazima idara hizo zifumuliwe hapo hapo” amesema Mwalimu.

Mbali na hilo aliwataka watangaza nia kutambua kuwa ni vyema wakawa na mawazo mapana.

“Iwapo Chadema itashika dola kuna nafasi nyingi kwa wale watia nia ambao watakuwa wameachwa,kuna nafasi za ukuu wa Mikoa, ukuu wa Wilaya na ukatibu mkuu na nafasi nyingine nyingi.

“Hakuna sababu yoyote ya mtangaza nia ambaye kura za maoni hazikutosha kwake akakata tamaa na badala yake anatakiwa kuungana na wenzanke ili kuhakikisha CCM inaondoka kadarakani na wao kupata kuongoza katika nafasi mbalimbali ndani ya serikali na ndani ya chama” amesema Mwalimu.

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amewataka watia nia wote kuzijua sheria mbalimbali za uchaguzi.

Akizungumza na watia nia wa kanda ya kati alisema mara nyingi vyama vya upinzania vimekuwa vikipoteza wagombea kutokana na kutokuzielewa vyema sheria za uchaguzi.

Lissu alisema wagombea wengi wa chama hicho walikuwa wakiwekewa mapingamizi na CCM kutokana na kushindwa kujiaza viruri fomu za ubunge.

Mbali na hilo alisema wale wote ambao watabahatika kupita katika kura za maoni wanatakiwa kuwa makini katika ujazaji wa fomu sambamba na kuwaelimusha mawakala ambao wanatakiwa kulinda kura katika vituo vya kupigia kura.

Mwanasheria huo alisema kwa kuwa hivi sasa Chadema kwa kushirikiana na Ukawa wana matarajio makubwa ya kushika dola ni lazima wagombea wote wakawa na elimu ya kutosha juu ya sheria mbalimbali zinazohusu uchaguzi.

“Kwa sasa Chadema imeisha shinda hoja ya mikutano ya hadhara na kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha inawatengeneza wapiga kura ili kuweza kuingia madarakani.

“CCM kwa sasa haina hoja yoyote yenye nguvu ambayo wanaweza kuitoa hadharani,na ndiyo maana wakifanya mikutano wanalazimika kuwasomba watu kwa mabasi,malori wakati Chadema wakifanya mikutano wananchi wanakuja wenyewe tofauti na CCM mabayo inalazimika kuwasafirisha watu na kuwagawia vitenge, pombe pamoja na kofia,” amesema Lissu.

Kutokana na hali hiyo ya mwamko ndani ya Chadema na watu kujitokeza kwa wingi kutangaza nia chama hakitafanya kosa kama lililotendeka kwa kumchukua mtu kama Shibuda ambaye hajui hata historia ya chama.

“Kwa sasa tunao watu wengi ambao ni makini wanakipenda chama hivyo hatakaye weza kupata nafasi ya kugombea ubunge ni mtu ambaye tayari chama kinamfahamu vyema na kukitumikia kwani makosa tuliyoyafanya kwa Shibuda hatuwezi kuyafanya tena”alisema Lissu,” amesema.

error: Content is protected !!