July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwakyembe: Tumedhibiti uchochezi wa kidini

Waziri wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Harrison Mwakyembe

Spread the love

DAKTA Harrison Mwakyembe- Waziri wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ameliambia Bunge kuwa, kutokana kuwepo kwa viashiria vya uchochezi wa kidini, wizara yake iliratibu kongamano la viongozi wa kidini katika nchi wanachama lililofanyika Septemba mwaka jana. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2015/15, Dk. Mwakyembe amesema lengo la kongamano hilo lilikuwa ni kujenga uelewa wa pamoja kuhimiza ushiriki wa viongozi dini katika Jumuiya.

Amesema kuwa, kongamano hilo liliazimia kushirikiana katika kushughulikia changamoto za kiusalama zinazotokana na uchochezi wa kidini kwa dini zote.

Kwa mujibu wa waziri, nchi wanachama zinatakiwa kuanzisha vituo vya kitaifa vya tahadhari ya majanga vya kuratibu na kutoa taarifa katika kituo cha kanda kilichopo jijini Arusha.

Kuhusu kupandisha hadhi hati za kusafiria ya Afrika Mashariki, alimesema kuwa, Novemba 2013, wakuu wa nchi wanachama walielekeza kukamilisha majadiliano ya kupandisha hadhi hati hiyo kuwa ya kimataifa ifikapo Novemba mwaka huu.

Hata hivyo, Dk. Mwakyembe amesema pamoja na mambo mengine katika kipindi cha mwaka jana na mwaka huu, kumeonekana kuwepo kwa matishio ya ugaidi.

“Kutokana na hali hiyo, wizara iliratibu na kushiriki katika mikutano ya tathmini ya utayari wa nchi wanachama kukabili mtandao wa kimataifa wa uhalifu ikiwa ni pamoja na ugaidi.

Kuhusu Mahakama ya Afrika Mashariki, Dk.Mwakyembe amesema ilipokea mashauri mapya 31 ambapo kitengo cha awali kilipokea mashauri 21na kitengo cha rufaa mashauri 10.

Amefafanua kuwa, mashauri 53 yalisikilizwa katika kitengo cha awali na kitengo cha rufaa.

Katika kutekeleza mambo mbalimbali, wizara hiyo imeomba Bunge liidhinishe bajeti ya Sh. 24.5 bilioni.

error: Content is protected !!