Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mwakyembe aiambia CCM ‘kujaa mikutanoni si ushindi’
Habari za Siasa

Mwakyembe aiambia CCM ‘kujaa mikutanoni si ushindi’

Spread the love

HARRISON Mwakyembe, aliyekuwa mbunge wa Kyela kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametahadharisha kwamba kujaa watu kwenye mikutano si hoja ya kushinda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kyela…(endelea).

Akizungumza na wanachama wa chama hicho kwenye uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo, jijini Mbeya amewataka wanachana hao kwenda kupiga kura tarehe 28 Oktoba 2020.

Amewataka wanachama hao kuacha kulumbana na badala yake, wasake kura za urais, mbunge na madiwani wa jimbo hilo.

Katika kura za maoni ndani ya CCM, Dk. Mwakyembe aliangushwa na Ally Mlaghila ambaye ndiye aliyepitishwa na chama hicho kugombea ubunge katika jimbo hilo.

“Ushindi haupatikani kwa wingi wa watu kujaa mikutano ya kampeni, bali kwa wingi wa kura,” amesema Dk. Mwakyembe.

Amesisitiza kuachana na dhana kwamba, ushindi tayari umepatikana kutokana na kutekelezwa kwa miradi mingi kwenye utawala wa Rais John Magufuli.

Hata hivyo, amewaomba wana Kyela kumpa kura Dk. Magufuli ambaye ni mgombea urais wa CCM, kutokana na juhudi zake za kuibadili Kyela na kuwa na taswira ya maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!