NAIBU Waziri wa Wizara ya Miundo Mbinu na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ametoa wito kwa jamii kuongeza juhudi katika kusoma vitabu ili kukuza maarifa.
Amesema usomaji wa vitabu unaisaidia jamii kupata mbinu mbalimbali za uongozi katika ngazi zote. Anaripoti Marry Victor…(endelea).
Mwakibete aliyasema hayo jana tarehe 15 Disemba, 2022 katika hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachohusu masula ya Uongozi kiitwacho (Leadership through my lenses).
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari na Teknolojia ya Mawasiliano Nape Nnauye; Mwakibete alimpongeza mtunzi wa kitabu hicho Violet Mordechai na kuongeza kuwa ili kupata viongozi wenye maono na ubunifu ni muhimu kusoma vitabu.
“Uongozi unatafsirika kwa njia tofauti, siri kubwa ni kupata vitabu vyenye simulizi za kusisimua za uongozi na kuvisoma kisha kuyaishi yale uliyoyasoma yakuongoze kwenye shughuli zako,” amesema.
Mwakibete aliongeza kusema: “Nimekisoma ni kitabu kizuri naomba nakala za kitabu hiki zisambazwe kwenye ofisi na taasisi za umma ili nao wayaishi haya yaliyoandikwa humu.
“Hongera sana Violet kwa uandishi na ubunifu mkubwa ulioutumia katika kuandaa kitabu hiki,” alisema Naibu Waziri Mwakibete ambaye kwenye hafla huyo alimwakilisha Waziri wa Habari na Tehama, Nape Nnauye.
Naye mtunzi wa kitabu hicho Violeth aliwashukuru waliohudhuria katika hafla hiyo: uzinduzi huo huku akisisitiza ujumbe uliomo katika kitabu hicho kwamba uongozi ni kuonesha njia.
Katika uzinduzi huo muongoni mwa vitabu vilivyokabidhiwa kwa Naibu Waziri viliendelea kuuzwa ndani ya ukumbi huku akitoa ahadi ya kuvitumia vitabu hivyo wakati wowote pale itakapohitajika katika taasisi za serikali na umma kwa jumla.
Leave a comment