Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwakibete ataka wahandisi SGR kupima vifaa vya ujenzi kikamilifu
Habari Mchanganyiko

Mwakibete ataka wahandisi SGR kupima vifaa vya ujenzi kikamilifu

Spread the love

 

NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete amewataka Wahandisi wa Shirika ya Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha vifaa vyote vinavyotumika katika ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR vinapimwa ubora wake kikamilifu kabla ya kutumika ili kuifanya reli hiyo kudumu kwa miaka 100. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Akizungumza jijini Mwanza baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo Sehemu ya Isaka hadi Mwanza yenye urefu wa Kilomita 249 Naibu Waziri Mwakibete, amesema thamani ya mradi huo itapimwa kupitia reli hiyo kufikia muda uliokusudiwa.

“Kwa fedha tulizowekeza hapa zaidi ya takribani trilioni tatu (3) sitegemei kama wataalam tutakubali nondo, simenti na vifaa vingine vitumike ambavyo havina viwango na niwakumbushe tu reli hii ikidumu mtakumbukwa na Taifa hili” amesema Mwakibete.

Mwakibete ameitaka TRC kupitia kitengo cha Masoko kuanza kufanya tafiti za kina kwa mzigo utakaosafirishwa kupitia reli hiyo kwani mikoa kama shinyanga kuna migodi na nchi Jirani kama Uganda zina mzigo mkubwa ambao zinaweza kuitumia reli hiyo kupitia Mwanza.

Aidha, Naibu Waziri Mwakibete ametoa rai kwa wananchi wanaoishi katika maeneo inapojengwa reli hiyo kujiepusha na vitendo vya wizi wa mafuta, simenti ili kutokwamisha miradi hiyo kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Meneja Mradi Sehemu ya Isaka hadi (Mwanza KM 249) Eng. Machibya Shiwa, amemhakikishia Naibu Waziri kuwa changamoto za upimaji zitaimarishwa pamoja na usimamizi kwani TRC imeongeza watalaam wa kutosha ili kuhakikisha maeneo yote yanasimamiwa.

Eng Machibya ameongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo mpaka mwezi oktoba 2022  umefikia asilimia 17 na kazi zinazoendelea kwa sasa ni kukamilisha kujenga tuta la reli ambayo ndio kazi kubwa kwenye ujenzi.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete yuko jijini Mwanza kwa ziara ya siku mbili (2) inayohusisha ukaguzi wa miradi na kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara ili kuona utendaji kazi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!