November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwakagenda aitibulia TBC1 bungeni

Spread the love

SHIRIKA la Utangazaji nchini (TBC1), limelalamikiwa kutoa matangazo yake kwa upendeleo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Sofia Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) leo tarehe 15 Mei 2019 mbele ya Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson wakati wa maswali bungeni, amehoji sababu za chombo hicho cha umma, kutoa habari zake kwa kubagua wapinzani.

Mbunge huyo akiomba mwongozo wa spika alisema kuwa, anasimama kwa kanuni ya 68(7).

“Mheshimiwa spika jana nilipokuwa nikiuliza swali la nyongeza, nilipata majibu kutoka kwa Waziri wa Habari na alijibu Waziri wa Mawasiliano na si vibaya waziri kulijibu.

“Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mwongozo wako, swali langu nilikuwa nikilaumu Televisheni ya Taifa kuonesha kwa upendeleo matangazo mbalimbali, hasa nilisema yakihusu vyama vya upinzani kwamba, habari zetu hazionyeshwi kwa usawa na vyama vingine.

“Mheshimiwa Naibu Spika, mheshimiwa waziri akinijibu alitaka  tumletee maudhui kuonesha ni jinsi gani anaweza kutusaidia ili habari zetu ziweze kutoka.

“Mheshimiwa Naibu spika, nataka nikukumbushe kwamba nikichukua sampo ndogo tu tarehe 9 mwezi huu, kambi rasmi ya upinzania tukitoa habari hapa bungeni TBC Taifa katika taarifa ya habari ya saa mbili, haikuweza kuonesha maoni ya Kambi Rasm ya Upinzani, wala michango ya wapinzani kwa muda mrefu sasa TBC imekuwa haioneshi habari za wapinzani.

“Mheshimiwa Naibu Spika, Naomba kiti chako kiweze kufuatilia suala hili na kujuhakikishia kwamba, tunapotoa maoni ya Kambi Rasm hapa bungeni iwe michango au hotuba ya kambi ya upinzani, TBC Taifa ambayo ni Televisheni ya Taifa inalipiwa kodi na Watanzania wote.

“Itoe usawa katika kuhabarisha jamii ninachoendelea hapa bungeni, haya ya nje tutaendelea kupambana huko nje kama ikibidi mheshimiwa spika tuone kama inafaha kwenda mahakamani, naomba mwongozo wa kiti chako,” amesema Mwakagenda..

Akitoa ufaganuzi wa mwongozo huo Naibu Spika amesema kuwa, ameombwa mwongozo na Sofia Mwakagenda kwa mujibu wa kanuni ya 68 (7), anaomba mwongozo wa jambo ambalo limetokea jana kwa swali lake la nyongeza ambalo alikuwa ameliuliza.

Kutokana na hali hiyo Naibu Spika amesema, kwa mujibu wa kanuni hiyo, jambo hilo halikutokea jana bungeni ila kutokana na hoja hiyo, serikali itakuwa imepata ujumbe huo na kwa maana hiyo ni vyema kulitafutia ufumbuzi kama kweli jambo hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara.

error: Content is protected !!