May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwakagenda ahoji ubovu barabara, Silinde amjibu

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Spread the love

 

SOPHIA Mwakagenda, Mbunge viti maalumu (asiye na chama), amehoji lini barabara ya Kiloba Ngugilo yenye urefu wa kilometa saba itajengwa ili kurahisisha mawasiliano ya kwenda kata ya Masukulu Rungwe. Anaripoti Jemima Samwel DMC … (endelea).

Ameyasema hayo leo Jumanne, tarehe 18 Mei 2021, katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo amesema, serikali inapaswa kuona umuhimu wa barabara hiyo kwa sabababu inafanya wanafunzi na wananchi wanaokwenda kata hiyo, kupata adha ya usafiri.

“Je ni lini barabara ya Kiloba-Njugilo yenye urefu wa kilomita saba itajengwa ili kurahisisha mawasiliano ya wananchi na wanafunzi wanaokwenda Kata ya Masukulu-Rungwe?

Sophia Mwakagenda

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Tamisemi, David Silinde amesema, barabara ya Kiloba-Njugilo ni barabara inayounganisha Kata mbili za Bujela na Masukulu.

“Kwa kutambua umuhimu wake, barabara ya Kiloba-Njugilo ipo kwenye hatua za uhakiki ili iweze kuingizwa kwenye Mfumo wa Barabara za Wilaya (DROMAS), ili iweze kupatiwa fedha za Mfuko wa Barabara kwa ajili ya matengenezo na ujenzi.

“Utaratibu wa kuingizwa kwenye mfumo wa barabara za Wilaya ukikamilika barabara hiyo itatengewa fedha kupitia fedha za Mfuko wa barabara (Road Fund) ili iweze kujengwa walau kwa kiwango cha changarawe na kuiwezesha kupitika katika majira yote ya mwaka,” amesema Silinde

Pia, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikali imejenga daraja la
Kigange linalounganisha vijiji vya Kiloba na Mwalisi kwa gharama ya Sh. 46.8 Milioni.

error: Content is protected !!