May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwadui FC waaga rasmi Ligi Kuu Tanzania Bara

Kikosi cha Mwadui FC

Spread the love

 

SASA ni rasmi klabu ya Mwadui FC imeshuka Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2020/21, baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0, nyumbani dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo ulipigwa kwenye Uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Msimu ujao mwadui watacheza Ligi Daraja la kwanza kwenye msimu wa 2021/22.

Kwa matokeo ya mchezo huo Mwadui FC itaendelea kusalia kwenye nafasi ya 18, wakiwa na pointi zao 19 katika michezo 30 waliocheza ambapo wameshinda michezo mitano, kufungwa mechi 22 na kutoka sare michezo minne.

Katika michezo minne Mwadui FC waliyosalia nayo hata wakishinda pointi 31, ambazo hazitaweza kuwasaidia kuepuka janga la kushuka daraja.

Katika Ligi Kuu msimu huu Mwadui FC imefungwa jumla ya mabao 56, katika michezo 30 waliocheza huku safu yao ya ushambuliaji ikifunga mabao 21.

error: Content is protected !!