December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mvutano waibuka mwenzake Mdee akihojiwa mahakamani, adai Wakili alimpania

Wakili wa Chadema, wakiongozwa na Peter Kibatala (katikati) wakiwa mahakamani

Spread the love

 

MVUTANO mkali umeibuka kati ya Wakili wa Chadema, Peter Kibatala na mleta maombi namba 11, Hawa Mwaifunga, kuhusu ajenda za kikao Cha Baraza Kuu la Chadema kilichofanyika tarehe 11 Mei, 2022. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni katika kesi Na. 36/2022, iliyofunguliwa na wabunge viti maalum 19 kupinga kufukuzwa ndani ya chama hicho, wakidai umauzi wa Chadema haukuwa halali kwa kuwa hakupewa nafasi ya kusikilizwa.

Mvutano huo umeibuka leo Alhamisi, tarehe 3 Novemba 2022, katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Cyphttps://www.youtube.com/watch?v=J5ULJXSTymA&t=78srian Mkeha.

Baada ya Wakili Kibatala kumuuliza Hawa kama alipewa nafasi ya kusema chochote katika kikao Cha Baraza hilo, ambapo mbunge huyo viti maalum alikataa kulijibu kwa kunukuu ajenda za Baraza Hilo.

Na kujibu kulingana na hati yake ya kiapo, akidai nafasi aliyopewa ni ya kuomba msamaha na si kusema chochote.

 

Mahojiano Yao yalikuwa kama ifuatavyo;

Kibatala: Ni kweli ama si kweli (minutes) ajenda hizo zinaonyesha ulipewa nafasi ya kusema chochote baada ya katibu mkuu kuwasilisha taarifa Kwa niaba ya Kamati Kuu. Ni kweli nafasi hiyo mlipewa?

Shahid: Hilo swali silielewi, jitahidi mpaka nielewe swali

Kibatala: Ni kweli ama si kweli hizo minutes zinaonyesha nafasi ya wewe kusema chochote ilitolewa kabla ya wajumbe hawajapiga kura?

Shahidi: Nafasi ya ku- apologize ndiyo nilipewa kabla ya wajumbe kupiga kura.

Jaji: Jibu swali

Shahidi: Ananilazimisha kusema anachotaka, Mimi sikupewa nafasi ya kusema chochote. Nilipewa nafasi ya ku- apologize.

Jaji: Kwa namna hiyo hamtakaa muelewane, lazima tusonge mbele. Msimamo wako (Kibatala ) walipewa nafasi ya kusema chochote kabla ya uamuzi kutolewa. Yeye (Hawa) msimamo wake chochote kilichotokea ni kupewa nafasi ya ku- apologize.

Kibatala: Wala Sina msimamo, namuuliza kwa mujibu wa minutes na sio msimamo wangu, ni kweli nafasi hiyo ilitolewa?

Shahidi: Kwa mujibu wa kiapo changu, nafasi iliyotolewa kwangu ni ku-apologize.

Kutokana na mvutano huo, Jaji Mkeha alimtaka Shahidi ajibu swali kama anavyoulizwa Kwa kuwa mawakili wake watapata nafasi ya kumuuliza maswali ya ufafanuzi.

Shahidi adai Wakili Kibatala alimpania

Kutokana na mvutano huo kudumu kwa dakika kadhaa, Jaji Mkeha aliwahoji Kwa nini wanakuwa wagomvi, ambapo Hawa alidai Wakili Kibatala alimpania.

Jaji: Leo mbona mnakuwa wagomvi sana?

Shahidi: Wakili alinipatia

Jaji: Na wewe umempania pia?

Shahidi: Na Mimi nikampania.

Hata hivyo, Wakili Kibatala amemaliza kumhoji maswali ya dodoso Hawa kuhusu malalamiko yake ya kufukuzwa Chadema kinyume cha Sheria.

Kesi hiyo imeahirishwa kwa muda wa saa moja ambapo ikirejea Hawa ataanza kuhojiwa maswali ya ufafanuzi na mawakili wake.

error: Content is protected !!