Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Mvutano waibuka kesi ya Sheikh Ponda
Habari Mchanganyiko

Mvutano waibuka kesi ya Sheikh Ponda

Sheikh Issa Ponda Issa, Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislam Tanzania akiwa mahakamani katika moja ya kesi zake
Spread the love

SERIKALI imeitaka Mahakama ya Rufani kuirudisha kesi ya jinai No. 245 ya mwaka 2012, inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda, katika Mahakama ya Kisutu ili atiwe hatiani. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Ombi hilo limeibuliwa leo tarehe 11 Juni 2019, katika mahakama hiyo baada ya kudaiwa kuwa, adhabu aliyopewa Sheikh Ponda ambaye ni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam ilikuwa ni kinyume cha sheria.

Kifungu kinachoelezwa kukiukwa ni 235 (1) cha mwenedno wa makosa ya jinai kwamba, Sheikh Ponda alihukumiwa kwenye Mahakamaa ya Kisutu bila kutiwa hatiani.

Awali, Sheikh Ponda alifunguliwa kesi ya jinai namba 245 ya mwaka 2012, ya kuvamia eneo la Markazi Chang’ombe, jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 9 Mei 2013, Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, alimuhukumu kifungo cha nje cha miezi 12 .

Sheikh Ponda kupita wakili wake Juma Nassoro, alikata rufaa kwenye Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo ambapo tarehe 27 Novemba 2014, Jaji Agostino Shangwa aliifuta hukumu hiyo na kueleza kuwa, Mahakama ya Kisutu haikumkuta na hatia yoyote na kwamba, madai ya kiwanja cha Chang’ombe kilichotajwa kuwa cha Waislam yalikuwa sahihi.

Leo mbele ya jopo la majaji  watatu wakiongozwa na  Jaji Stella Mugasha, Fredrick Wambali na Rehema Kerefu wamesikiliza rufaa ya serikali ya kupinga ubatilishwaji wa hukumu ya Sheikh Ponda iliofanywa na Mahakama Kuu.

Upande wa mrufaniwa umewakilishwa na Wakili Nasorro, aliyesaidiwa na wakili Fauzia Kajoki huku upande wa serikali ukiwakiliswa na Wakili Nassoro Katuga.

Wakati rufaa hiyo ikisikilizwa, majaji waligundua kasoro ya kisheria katika Hukumu ya Mahakama ya Kisutu ambapo Hakimu Nongwa alitoa uamuzi kinyume na kifungu 235 (1) cha Mwenendo wa makosa ya jinai, kutokana na kutoa adhabu kwa mtuhumiwa bila ya kumtia hatiani.

Wakili Katuga alitaka hukumu ya Mahakama ya Kisutu ifutwe na faili lirudishwe mahakamani hapo (Kisutu), ili mahakama hiyo ikamtie hatiani upya mrufaniwa (Sheikh Ponda) na kuanza kutumikia adhabu kuanzia hapo.

Malumbano ya hoja kwa mawakili wa pande zote mbili yalibuka mahakamani hapo ambapo wakili Juma Nassoro, ameieleza mahakama hiyo kuwa, kisheria hukumu ilishatolewa na mrufani (Sheikh Ponda)  ameshatumikia adhabu.

Nassoro ameeleza mahakama kuwa, hukumu haiwezi kukamilika bila ya kumtia hatiani mshitakiwa au amwachie huru ili haki ionekane imetendeka.

Na kwamba, mshitakiwa anapaswa kuachiwa huru moja kwa moja akaendelee na shughuli zake, na si kumrudisha upya Kisutu ili akatiwe hatiani upya.

Ameeleza sababu ni kuwa, mahakama ikiamua kumrudisha Kisutu ili akatiwe hatiani, maana yake mahakama itakuwa imethibitisha hukumu ile ni halali isipokuwa iongezewe sehemu ya kumtia hatiani mshitakiwa jambo ambalo pia si sawa kisheria.

Mahakama baada ya malumbano hayo, imepanga kutoa uamuzi kwa tarehe nyingine ambayo itawaarifu mawakili wa pande zote mbili.

Mwaka 2012, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) liliuza eneo lilitarajiwa kujengwa Chuo Kikuu cha Kiislamu, Markaz Chang’ombe katika Wilaya ya Temeke.

Sheikh Ponda na Waislamu wengine walipinga vikali kitendo cha kutaka kuuza eneo hilo, ndipo tarehe 12 Oktoba 2012 walijikusanya katika eneo hilo kupinga kitendo hicho kwa kujenga msikiti katika eneo hilo ulioitwa Hassan Bin Ameir.

Katika eneo hilo, polisi walivamia na kurusha mabomo ya machozi na kuwapiga masheikh na wafuasi wao ambapo Sheikh Ponda na wafuasi wengine 49 walikamatwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

Habari Mchanganyiko

Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Greyhorse zasaini mkataba wa bil.7.4

Spread the loveTAASISI ya Mwalimu Nyerere (MNF) imesaini mkataba wa miaka 10...

error: Content is protected !!