November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mvutano wa hoja za mawakili waahirisha uamuzi kesi kina Mbowe

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema akiingia mahakamani

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi iliyopo Mawasiliano jijini Dar es Salaam, imeahirisha kutoa uamuzi madogo katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake hadi kesho Jumatano tarehe 17 Novemba 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni uamuzi unaohusu pingamizi lililowekwa Ijumaa iliyopita 12 Novemba 2021 na mawakili wa utetezi, wakitaka shahidi wa pili wa jamhuri, Askari Mpelelezi, Ricardo Msemwa, aondolewe kuwa shahidi.

Pingamizi hilo, liliwekwa baada ya shahidi huyo kukutwa akiwa na simu, kalamu, karatasi na diary kwenye kizimba wakati akitoa ushahidi wake.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya ugaidi ni Halfan Hassan Bwire, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya ambao walikuwa makandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Siku nzima ya jana Jumatatu, mawakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya na Peter Kibatala walichuana na wale wa mashtaka kumpinga shahidi huyo huku wale wa jamhuri wakiiomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo.

Leo Jumanne, wakati mawakili wa pande zote pamoja na washtakia wakiwa mahakamani na Jaji Joachim Tiganga akisubiriwa kutoa uamuzi, amesema jana jioni “niliahirisha shauri, nikasema nitasoma uamuzi leo. Lakini kutokana na wingi wa hoja naomba muda zaidi mpaka kesho nikakamilishe kuandika uamuzi.”

“Naomba radhi kwa ahirisho hili ambalo hatukulitarajia,” amesema Jaji Tiganga na kuongeza:

“Kama nilivyosema kwamba naahirisha shauri mpaka kesho, upande wa mashitaka mtamleta shahidi atakaa kizimbani na ataendelea kutoa ushahidi. Naahirisha mpaka kesho saa 3 asubuhi..”

Katika pingamizi hilo,  upande wa utetezi uliiomba mahakama hiyo imuondoe, Msemwa, wakidai amekosa sifa za kuwa shahidi kutokana na kukutwa na simu, diary na kalamu wakati akitoa ushahidi katika kizimba cha shahidi.

Kesi hiyo ndogo iliibuka kufuatia mapingamizi ya utetezi dhidi ya maelezo ya onyo ya mshitakiwa Ling’wenya yasipokelewe mahakamani hapo wakidai mtuhumiwa hakuandikwa maelezo katika kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, tarehe 7 Agosti mwaka jana bali alisainishwa karatasi yenye maelezo yaliyodaiwa kuwa ya kwake katika Kituo cha Polisi cha Mbweni jijini humo.

error: Content is protected !!