Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mvutano: Trump anataka vita, bunge linamgomea
Kimataifa

Mvutano: Trump anataka vita, bunge linamgomea

Spread the love

AZIMIO la kumzuia Rais wa Marekani, Donald Trump kuanzisha vita na Iran, limezua mvutano baina ya Chama cha Democrats na Republicans. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Tayari Bunge la Wawakilishi nchini humo, lenye wawakilishi wengi wa chama pinzani cha Democrats, limepitisha azimio la kumzuia Rais Trump, kupigana vita na Irani. Azimio hilo limepitishwa kwa kura za ndio 224 dhidi ya kura za hapana 194.

Baada ya azimio hilo kupitishwa, Chama cha Rais Trump cha Republicans, kimetangaza kukwamisha azimio hilo, katika kura zitakazopigwa kwenye Bunge la Seneti, ambako kuna wawakilishi wengi wa chama hicho.

Kevin McCarthy, Kiongozi wa Republican ndani ya Bunge la Wawakilishi, amekosoa azimio hilo, akisema kwamba lilikuwa sawa na tamko kwa vyombo vya habari, hivyo halitafanyiwa kazi.

Pia, Rais Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter, amewasihi wawakilishi wa Republican katika Bunge la Seneti, kupiga kura za kukataa azimio hilo.

Rais Trump amesema, taarifa za kijasusi za taifa hilo zinaonesha kwamba, Iran inapanga kushambulia Ubalozi wa Marekani uilioko Baghdad nchini Iraq.

Dhumuni la azimio hilo ni kumdhibiti Rais Trump kutumia Jeshi la Marekani dhidi ya Irani, pasina idhini ya baraza hilo la wawakilishi nchini Marekani.

Hata hivyo, azimio hilo limeafiki Rais Trump kufanya mashambulizi bila kibali cha baraza hilo, pindi Marekani itakapo hitaji kujilinda dhidi ya mashambulizi kutoka Iran.

Mvutano baina ya Iran na Marekani umeshika kasi baada ya Jenerali Qasem Soleiman, aliyekuwa kiongozi mwandamizi wa jeshi nchini Iran,  kuuawa na Wanajeshi wa Marekani katika shambulio la anga, mjini Baghdad nchini Iraq, Ijumaa ya tarehe 3 Januari mwaka huu.

Baada ya Jenerali Soleiman kuuawa, Iran ilianza kulipa kisasi dhidi ya Marekani, kwa kushambulia kwa makombora kambi zake mbili zilizoko nchini Iraq.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

Kimataifa

Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki

Spread the loveKIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anadaiwa kupanga kumfumkuza...

error: Content is protected !!