Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mvulana kidato cha 4 auawa kwa kuvamia bweni la wasichana
Kimataifa

Mvulana kidato cha 4 auawa kwa kuvamia bweni la wasichana

Spread the love

 

MWANAFUNZI mmoja wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya wavulana ya Gathiruini, kaunti ya Kiambu nchini Kenya, amefariki dunia baada ya kuvamia bweni la shule ya wasichana iliyopo jirani na kushambuliwa kwa fimbo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), George Kinoti amesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 kwa kushirikiana na wenzake wengine watano walitoroka shuleni kwao muda ya saa kumi asubuhi ya kuamkia Alhamisi jana na kuelekea katika shule ya Sekondari ya wasichana Komothai iliyo jirani na shule yao.

Kinoti amesema vijana hao sita hao walipofanikiwa kuingia ndani ya shule hiyo ya wasichana, walinyata hadi kwenye bweni mojawapo na kuingia ndani.

“Haijathibitishwa wazi kile ambacho vijana hao walikuwa wameenda kufanya pale ila mpango wao uligonga mwamba baada ya baadhi ya wasichana kuwaona na kupiga yowe mara moja.

“Wanafunzi wengine pamoja na walimu na walinzi walielekea eneo la tukio kujionea kilichokuwa kinaendelea ila wavulana watano kati ya sita waliokuwa wameingia kwenye bweni hilo, walitoroka na kurudi kwa shule kwao huku wakimuacha mwenzao mmoja nyuma.

“Mvulana ambaye aliachwa nyuma alikamatwa na kupewa kichapo cha mbwa koko na kumsabishia majeraha yaliyomuacha katika hali mahututi,” amesema.

Amesema baada ya hapo alikimbizwa katika hospitali ya Kigumo ambako alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata.

DCI huyo ametoa onyo kali kwa umma kuacha kuchukua sheria mikononi na badala yake kuwaruhusu washukiwa wajibu mashtaka yao mbele ya mahakamani.

Aidha, Mlinzi wa shule hiyo ya wasichana, George Karanja amesema tayari wapelelezi wamefika kwenye eneo la tukio na kuchukua fimbo zilizoaminika kutumika kushambulia marehemu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!