July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mvua zaleta kizaazaa Arusha

Mafuriko Arusha

Spread the love

MVUA zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Arusha, zimeanza kuleta madhara mbalimbali katika baadhi ya mitaa ikiwemo mifugo kufa na makaravati kubomoka. Anaandika Doreen Aloyce, Arusha …(endelea). 

Wananchi wa Mtaa wa Kanisani katika kata ya Sokoni 1, ni moja ya mitaa ambayo imeathirika hasa kwa upande wa miundombinu ya barabara, na hivyo shughuli zao kukwama.

Wakizungumza na MwanaHALISIOnline kwa nyakati tofauti, wamesema kuwa mtaa wao umesahauriwa na Manispaa ya Jiji kwani miundombinu hairidhishi hali inayofanya mtaa kutokuwa na maendeleo. 

“Mvua hizi zinazoendelea kunyesha, mbali na kusomba mifugo yetu, lakini pia jiji limeshindwa kukusanya taka kwa ufasaha na hivyo wafanyabiashara kado ya barabara tupo katika hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza kutokana na taka hizo kutapanywa na mvua,” wanalalamika. 

Wanaongeza kuwa, “ukosefu wa mitaro ya kutiririsha maji taka pia ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa barabara.”

Mwenyekiti wa mtaa huo, Madaraka Sokya (Chadema), ameliambia gazeti hili kuwa, amekuwa akipokea kero za wananchi kuhusu uchelewaji wa manispaa kuzoa taka kando ya barabara licha ya kukusanya fedha kwa wafanyabiashara. 

Ameiomba manispaa ya jiji kuonyesha ushirikiano na wananchi kwa kujenga mitaro ya kupitisha maji, kuleta gari ya kumwaga vifusi kwa ajili ya kuziba mapengo ikiwa ni njia ya kunusuru maisha ya wananchi.

error: Content is protected !!