January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mvua yatesa familia 360 Morogoro

Spread the love

MVUA iliyoambatana na upepo mkali imeezua na kubomoa nyumba na kusabisha hasara kubwa kwa zaidi ya familia 360 katika wilaya mpya ya Malinyi mkoani Morogoro. anaandika Christina Raphael … (endelea).

Mvua hiyo ilinyesha jana, na kwa mujibu wa Said Msomoka, mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, athari hizo zimeumiza wakazi wapatao 1,600 katika vijiji mbalimbali.

Baadhi ya wakazi hao wasio na makazi wamepata hifadhi kwenye majengo ya shule na mengine ya umma. Wengine wanatumia vibanda vyenye hadhi ya chini.

Mvua hiyo, ambayo pia ilikuwa na radi, imeangusha miti mikubwa ya asili ambayo imeziba barabara na kufanya wasafiri na watumiaji wa barabara kuu ya Lupiro-Mtimbira hadi Malinyi kuchangishana ili kupata fedha ya kulipa wenye vifaa maalum vya kukatia miti hiyo.

error: Content is protected !!