April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mvua yachafua hali ya hewa, DART yasitisha usafiri

Spread the love

MVUA iliyoanza kunyesha mfululizo kuanzia alfajiri ya leo tarehe 17 Desemba 2019, imeleta adha kwa wakazi Jiji la Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mvua hiyo imesababisha nyumba zilizoko mabondeni kujaa maji na barabara kutopitika, hali iliyopelekea baadhi ya wananchi kukwama kuendelea na shughuli zao za kijamii.

Miongoni mwa maeneo hususan kwenye barabara, yaliyoathiriwa na mvua hiyo ni pamoja na barabara ya Morogoro maeneo ya Jangwani,  baadhi ya sehemu katika Barabara ya Mandela.

Na barabara ya Shekilango maeneo ya daraja la Mugabe, barabara ya Kawawa maeneo ya Kinondoni Mkwajuni.

Kufuatia adha hiyo, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART),  imesitisha safari zake kutoka Kimara na Morocco kuelekea Kivukoni, Kariakoo na Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa ya wakala huo iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa twitter, wasafiri wanashauriwa kutumia usafiri mbadala ili kufika maeneo hayo.

error: Content is protected !!