Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Mvua ya magoli dabi ya Mbeya, sare zatawala
Michezo

Mvua ya magoli dabi ya Mbeya, sare zatawala

Spread the love

KIPUTE cha Ligi Kuu Bara kimeendelea tena leo tarehe 3 Oktoba 2021 kwa mechi tatu kupigwa katika viwanja vitatu tofauti na kushuhudia timu zote sita zikiondoka na alama moja. Anaripoti Kelvin Mwaipngu…(endelea)

Pia dabi ya Mbeya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka hususani mkoani humo kati ya Mbeya City na Mbeya kwanza nayo imemalizika bila mbabe.

Mechi hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa Sokoine Stadium mkoani Mbeya imeshuhudia mvua ya magoli kwa mara ya kwanza tangu msimu huu wa ligi uanze.

Katika mchezo huo Mbeya City ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 44 ya mchezo kupitia kwa Paul Nonga, kisha Richardson Ngodya akaandika la pili dakika ya 75.

Hata hivyo, Mbeya kwanza walijibu mashambulizi kupitia kwa Castory Mhagama aliyeingiza kambani mabao yote mawili dakika ya 77 na dakika ya 86.

Hadi dakika 90 zinakatika vita hiyo ya ndugu haikuwa na mbabe huku timu zote zikifikisha alama nne kila moja.

Mtanange mwingine ulikuwa kati ya Mtibwa Sugar na Maafande wa Tanzania Prisons ambapo mechi hiyo imemaliza kwa sare tasa yaani 0-0 kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Mtibwa Sugar kwa usajili walioufanya kabla ya msimu huu kuanza walikuwa wanatabiriwa kufanya makubwa lakini hadi sasa katika mechi mbili za kwanza wameambulia alama moja pekee.

Sare nyingine ya tatu imepatikana katika Uwanja wa Ilulu mjini Lindi ambapo wenyeji Namungo FC wamefungana 1-1 na Kagera Sugar ya Bukoba mkoani Kagera.

Bao la Namungo FC leo limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Relliant Lusajo dakika ya  53, kabla ya mshambuliaji mwingine, Mbaraka Yussuf kuisawazishia Kagera Sugar dakika ya 71.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!