June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mvua kuendelea kutikisa Dar hadi Mei

Matukio ya mafuriko Dar es Salaam

Spread the love

MVUA kubwa na fupi zitaendelea kunyesha kati ya Machi hadi Mei mwaka huu. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Tahadhari inatolewa zaidi katika ukanda wa Pwani umaojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, Tanga na visiwa vya Pemba na Unguja.

Dk. Agnes Kijazi – Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) anasema, “kutakuwa na mawingu makubwa huku mvua ikiendelea kuimalika kati ya leo hadi 25 Machi mwaka huu. Wananchi wanapaswa kuchukua hatua”.

“Tulitoa tadhari iliyoishia jana. Tumetoa tena tahadhari kwa siku tatu zaidi. Kuna uwezekano wa kupata mvua kubwa zinazofikia au kuzidi milimita 50 kwa masaa 24,” amesema Kijazi.

Wakati tahadhari hiyo ikitolewa, tayari vyombo vya habari vimemnukuu Kamanda wa Polis Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, ikisema hadi kufikia jana “watu watano wamefariki dunia na wengine kadhaa kulazimika kuyahama makazi yao kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar Salaam.

Aidha, 4 Machi mwaka huu, watu 38 walifariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa vibaya kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha na kusababisha mafuriko katika Kijiji cha Mwakata, Kata ya Isaka Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Samuel Sitta – Waziri wa Uchukuzi amesema “taarifa za hali ya hewa ni muhimu ili kukabiliana na changamoto hizi”.

“Hivyo ni muhimu jambo la kuzingatiwa kwa watoa maamuzi kuhakikisha kwamba wanapata uelewa wa kutosha wa masuala ya hali ya hewa na namna ya kutumia taarifa hizi katika kutoa maamuzi,” amesema Sitta.

Leo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) pamoja na nchi wanachama jumuiya ya kimataifa ikiwemo Tanzania zinaadhimisha siku ya hali ya hewa duniani, kaulimbi ya mwaka huu ikiwa “Uelewa wa hali ya hewa kwa maamuzi stahiki”.

error: Content is protected !!