May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mvua kubwa kunyesha mikoa 7 Dar ikiwemo

Mvua kubwa ikinyesha

Spread the love

 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kunyesha mvua kubwa kwa siku tano kuanzia leo Jumapili, tarehe 18 Aprili 2021, katika maeneo ya mikoa ya Lindi, Morogoro, Pwani (ikihusisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam na Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa iliyotolewa na TMA, imetoa angalizo la upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0, kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya bahari ya Hindi.

Mikoa hiyo ni ya; Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

loop

error: Content is protected !!