August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mviwata waililia serikali ya JPM

Shamba la mahindi

Spread the love

MTANDAO wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), umeazimia kuishauri Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Uvuvi kutowatoza gharama wakulima wanaoshirikia maonesho ya sikukuu ya wakulima, anaandika Mwandishi Wetu.

Hayo yalisemwa juz na Ofisa uwezeshaji kiuchumi wa MVIWATA, Nickson Elly wakati akisoma mapendekezo ya warsha ya wadau wa mtandao kutoka mikoa ya Iringa, Njombe na wilaya mbalimbali za Morogoro iliyofanyika kwenye viwanja vya maonesho ya wakulima.

Elly aliyataja mapendekezo mengine kuwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa benki za kilimo kuwafikia wakulima walipo na kuondoa shida ya kupata huduma.

Ametaja mapendekezo mengine kuwa ni kuhakikisha MVIWATA kwa kushirikiana na vikundi husika wanakuwa na sauti ya pamoja ya kusemea changamoto zinazowakabili na hivyo kuweza kupatiwa ufumbuzi kadri wanavyoweza.

Awali Mkurugenzi wa mtandao huo, Stephen Ruvuga alisema, atahakikisha wakulima wanaingi bure uwanjani kwani wao ndio weenye sherehe na hivyo suala la kulipia viingilio lisiwaguse.

Aidha, Ruvuga alisikitishwa na kitendo cha wanunuzi kutotumia vipimo halali katika manunuzi ya mazao ya wakulima na kusema kuwa kitendo hicho ni wizi kama ulivyo wizi mwingine.

error: Content is protected !!