February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

MV Kigamboni, MV Kazi kusitishwa huduma zake

Spread the love

IWAPO Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) pia Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) watashindwa kuboresha usafiri wa maji, vyombo hivyo vitasitishwa kuendelea kutoa huduma. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 26 Septemba 2018 na Sara Msafiri, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni wakati wa ziara yake.

Sara amesema, hatua hiyo itachukuliwa kwa kuwa, amebaini upungufu mkubwa katika uendeshaji wa kivuko hicho.

Akina na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya yake Sara amesema, kwa kuwa daraja la Nyerere lipo hakutakuwa na sababu ya kuendelea na uendeshaji vivuko huvyo kama maagizo ya uboreshaji hayatofanyiwa kazi.

“Kuna tatizo kwenye usimamizi na uendeshaji, hakuna kamera za usalama lakini pia hakuna hata namba za dharura ndani ya kivuko,” amesema.

“Tumebaini mapungufu mengi sana, nimetoa maelekezo kama hayatafanyiwa kazi tutafunga kwa sababu tuna daraja letu la Mwalimu Nyerere tutalitumia.

error: Content is protected !!